topbella

faidika Rafiki kwa
kutembelea Blog
ya
Kijanja.
.

WAHI

Eleza Hisia zako!

kama unajambo unataka liwekwe katika page hii tutumie barua pepe katika jmbewa@gmail.com

[hisia za Zawadi Mbewa]
Maisha yana changamoto kubwa sana ambayo mimi na wewe yatubidi kukabiliana nazo ili tuweze kufanikiwa katika maisha haya. jambo la busara na la muhimu ni kuto kukata tamaa kwa kile tunachonuia kufanya kwa kutarajia ni njia ya kuweza kutuletea Maendeleo katika jamii yetu.
Ni mambo mengi yanafanyika na sisi tumebaki kuwa watu wakutoa lawama kwa viongozi wetu lakini yatu pasa kutambua ya kwamba Watanzania waleo tunaitaji kuwa na moyo wa kizalendo na kuwa na upendo baina yetu ambapo kwa kufanya hivyo basi mambo mengi ambayo tunatamani na sisi Taifa letu la Tanzania liyafikie basi yatafanikiwa ni jambo la kusikitisha kwamba Watanzania wengi sasa moyo wa kizalendo umekufa ndiyo maana mambo mengi yasiyo kuwa ya kawaida yamekuwa ya kifanyika katika taifa hili masikini lakini ni wajibu wa mimi na wewe kusimama kikamilifu katika nafasi tulizo nazo katika jamii hii na kuhakikisha ya kwamba haki na usawa vinatendeka, kwa kufanya hivyo tutafanya nchi hii iwe sehemu nzuri kwa kuishi na hatimaye maendeleo yatakuja.
Watanzania wenzangu tuache ile tabia ya kutaka kufanikiwa kwa njia ya mkato kwa mambo mbalimbali tunayo yafanya kilasiku katika maisha yetu kwani kwa kufanya hivyo ndio maana jamii yetu inazidi kuwa ni jamii yenye tabaka lenye utamaduni wa kupata huduma mpaka utoe chochote ambapo sasa kuna watanzania wenzetu ambao wanahitaji huduma ambazo ni haki yao lakini hawapati hiyo fursa kwa sababu ya kukosa hicho chochote.
kwahiyo ewe kijana mwenzangu kuwa mjanja wa karne uifanye Tanzania ni sehemu bora kwa kuishi kwa kuanza kuonesha Uzalendo wako!
Tukisimamia kikamilifu na kiuaminifu kwa kuwa na moyo wa Upendo baina yetu basi kila janbo linawezekana!



Na Jayson!!
jamani pic ya kuagana na walimu wa BTP!

About Me